Wednesday, July 10, 2013

ARSENAL KUMKOSA LUIS SUAREZ REAL MADRID WAINGILIA KATI DILI HILO

WAINGILIA KATI DILI HILO


REAL MADRID wako tayari kuitibulia Arsenal katika dili lao la kumnasa Luis Suarez.

Mshambulia huyo wa Liverpool anayetaka kuondoka alifichua kuwa ana machaguo mawili au matatu lakini akazibeza ripoti za yeye kujiunga na Chelsea.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amejipanga kupeleka ofa ya milioni 40 kwa nyota huyo – siku chache tu baada ya Liverpool kuitupilia mbali ofa ya pauni milioni 30 kutoka kwa Arsenal.

Suarez alifafanua: “Wakala wangu ndio kila kitu, anajua nini nachotaka.

“Inavutia kugundua kuwa timu kama Arsenal inathamini mchango wangu.

“Kwasasa kuna sehemu mbili au tatu na klabu yangu inajua”