Sunday, August 3, 2014

Sierra Leone yatangaza hali ya dharura kutokana na Ebola

Daktari akionesha vipimo vya ugonjwa wa Ebola

Rais wa Siera leone Ernest Bai Koroma ametangaza hali ya dharura nchini humo ili kusaidia nchi hiyo kukabiliana na mlipuko mbaya kuwahi kutokea wa virusi vya Ebola.
Katika hotuba yake kwa taifa, bwana Koroma alisema serikali inaweka karantini katika maeneo yaliogundulika na ugonjwa huo, ikidhibiti mikusanyiko ya hadhara, ikiangalia nyumba hadi nyumba kuwatambua watu walioathirika na kutathmini utaratibu kwa wasafiri kwenye uwanja mkuu wa ndege nchini humo.

Hatua hiyo itafanywa kwa siku 60 hadi 90. Rais huyo alisema Sierra leone ipo katika mapambano makali na kwamba kusambaa kwa Ebola ni zaidi ya nchi moja au jamii ili kuweza kukabiliana nayo.

Bwana Koroma alisema atakwenda nchini Guinea kesho kukutana na viongozi wenzake wa Guinea na Liberia. Pia aliakhirisha safari yake wiki ijayo kuelekea Washington ambako rais Baraka Obama ni mwenyeji wa mkutano unaowajumuisha viongozi kutoka mataifa barani Afrika