Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
Tukio hilo la
aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huu katika zahanati hiyo ambayo
jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya
Global Publishers ikiwa katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo
polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi
madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.
Daktari
Shengena alipoona kamera ya OFM alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa
askari ndani ambapo walitumia nguvu za ziada kuwadhibiti vyema na
kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo mwenzake ambaye naye alinaswa
akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya kuchomolea mimba akiwa amevificha
kwenye mfuko wa rambo.
Madaktari wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
Baada ya
maafande kuwaweka chini ya ulinzi, madaktari hao walizua kituko kufuatia
kuzitupa chini shilingi 40,000 walizopewa na denti huyo kama malipo ya
kazi hiyo wakidhani ni za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
‘Takukuru’.
kiasi cha fedha cha Shillingi arobaini elfu walicholipwa madaktari kwa ajili ya kufanikisha zoezi la utoji mimba.
Wakizungumza na
waandishi wetu baada ya kuulizwa nini kilikuwa kikiendelea chumbani
humo, Dokta Chacha alidai kuwa mgonjwa huyo ana tatizo kwenye kizazi
hivyo alikuwa akitaka kusafishwa na si kutoa mimba maelezo yalikosolewa
na denti huyo aliyedai kuwa alikwendwa kwa mapatano ya kumchoma mimba
ili akaendelee na masomo chuoni.
Binti (denti) aliyekusudiwa kutolewa mimba.
Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa
va kutolea mimba kwenye mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti
huyo alifuata taratibu zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa
kuonesha risiti au cheti cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya
matibabu.
Zahanati iliyotumiwa na madaktari hao katika jaribio la utoaji mimba.
Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM
na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta
kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na
manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa
ushahidi.Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.
CREDIT: GPL