Saturday, July 5, 2014

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha afikishwa mahakamani



MKuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa  Johannes Monyo na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha, kujibu mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 6.2.

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Muspher Siyani, mwendesha mashitaka wa serikali, Adam Kilongozi, akiwa na mwendesha mashitaka wa Taaisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Amidu Simbano, alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa wanashitakiwa kuhujumu uchumi, ambapo Septemba 30 mwaka 2011 katika Chuo cha Uhasibu, akiwa Mkuu wa Chuo na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, walitumia nafasi zao vibaya kubadilisha matumizi ya ‘Solar Power Back Up Kit’ yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 6.2 kwa matumizi yake binafsi kama Mkuu wa Chuo.

Alidai kuwa kosa la pili  washitakiwa hao Julai 29, 2011 katika Chuo cha Uhasibu, wakiwa kama wajumbe wa Bodi ya Manunuzi wa Chuo hicho, waliidhinisha matumizi ya solar Power Back Up Kit ya thamani ya Sh. milioni 6.2 na kuwapatia kampuni ya Helvetic Solar Contractors na kujipatia sola hiyo isivyo halali.

Kosa la tatu wameshitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka ambapo Faraji Mnyepe kama Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu, Jerome Augustino na Honory Mkelemi  wanashitaki wakati ya Novemba mosi mwaka 2011 na Novemba 30 mwaka huo, walifanikisha utekelezaji wa malipo ya Shilingi milioni 6.2 katika kampuni ya Helvetic Solar Contractors na kunufaika isivyo halali.

Aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa kosa la nne wanashitakiwa kwa kusababishia hasara serikali , ambapo mnamo Julai 26 mwaka 2011 na Novemba 30 mwaka 2011 katika chuo hicho  walisababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi milioni 6.2