KATIKA staili ya aina yake ya kuuaga mwaka na kuukaribisha 2014, mtangazaji Peniela Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa Nasib Abdul ‘Diamond’ alipewa zawadi ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii nyumbani kwake Mwananyamala Mwinjuma alikohamia hivi karibuni, baada ya watu wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema Sepetu, kufika hapo wakiwa na ‘mzigo’ huo uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua.
Juu ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji huyo kulikuwa na maandishi yaliyomsuta na kumtaka kuachana na tabia ya kuchukua mabwana wa rafiki zake pamoja na dada zake, hali inayoonyesha kuwa waliompelekea ujumbe huo ni wabaya wake.
Juhudi za kumtafuta Penny kuzungumzia tukio hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mtamboni