Video
ikimwonyesha Kamanda Kova wakati akiongea na wanahabari kuhusu matukio
mbalimbali ya kihalifu na watuhumiwa waliokamatwa na Jeshi la Polisi
wakiwemo waliomshambulia Dk. Mvungi.
Kamanda Suleiman Kova akiongea na wanahabari kuhusu wahalifu mbalimbali waliotiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
Baadhi ya vitu walivyokutwa navyo wahalifu katika matukio mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Stori: Jelard Lucas na Chande Abdallah
WATU 6 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio la
kumshambulia Dkt. Sengondo Mvungi aliyevamiwa na majambazi nyumbani
kwake Kibamba Msakuzi juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Selemani Kova amesema katika operesheni maalum
iliyofanywa na jeshi la polisi, wamefanikiwa kuwakamata watu sita ambao
majina yako yamehifadhiwa kwa sababu za usalama. Aidha Kamanda Kova
aliongeeza kuwa bado hawajapata uthibitisho kamili juu ya sakata hilo na
uchunguzi unaendelea kuwabaini wahusika halisi wa shambulio hilo |