Thursday, November 7, 2013

MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI , ABSALOM KIBANDA AANGUA KILIO UKUMBINI KABLA YA KUKABIDHIWA TUZO

Mshindi  wa  tuzo ya Daudi Mwangosi, Absalom Kibanda ambaye ni mwenyekiti wa jukwaa la  wahariri akibembelezwa na mkewe  baada ya  kuangua kilio ukumbini mara baada ya kutangazwa mshindi  wa tuzo hiyo leo jijini Mwanza
Kibanda  akiendelea  kuliza  wajumbe wa mkutano mkuu  wa UTPC leo
Kibanda akielekea  kupokea  tuzo huku akila kwa uchungu


Kibanda akibembnelezwa na mmoja kati ya majaji  wa tuzo hiyo


Mgeni  rasmi katika hafla  hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi Bw  Tido Mhando  wa tatu  kulia  akimkabidhi mshindi  mfano  wa hundi ya Tsh milioni 10,  katikati ni mjane  wa Mwangosi  Itika Mwangosi  wa kwanza  kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na  rais  wake  Keneth Simbaya
  • Na  Francis Godwin Blog Mwanza
 Mshindi  wa tuzo  yakishujaa na uandishi  uliotukuka  ya  Daudi Mwangosi Absalom Kibanda  leo  amewaliza  wajumbe  wa mkutano mkuu  wa umoja  wa vilabu  vya  waandishi  wa habari nchini (UTPC)  baada ya  kushindwa  kusimama  kupokea  tuzo   hiyo yenye  thamani  ya Tsh  milioni 10 na badala  yake  kuangua  kilio  kwa uchungu ukumbini hapo.
Tukio  hilo ambalo ni la kwanza katika  histori  ya  washindi wa tuzo mbali mbali kutokea nchini  limetokea leo katika Hotel la JB jijini Mwanza  wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hiyo iliyotolewa na UTPC.
Kibanda ambae muda  wote  alionekana kutulia katika nafasi yake hadi pale jiji mkuu wa tuzo hiyo mwanahabari maarufu nchini Tanzania Hamza kasongo kupita mbele na kusoma  sifa  za mshindi wa tuzo  hiyo na kumwita  mmoja kati ya majaji  kutaja  jina la mshindi .
Baada  ya  kibanda kutangazwa mshindi hakuweza kuonyesha furaha kama ilivyo kwa washindi  wengine na badala yake kuanza  kulia kwa uchungu kiasi cha baadhi ya wajumbe ukumbini hapo akiwemo makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanjo kuungana nae  kuangusha  chozi  ukumbini hapo na kufuatiwa na wajumbe mbalia mbali akiwemo mjane wa Mwangosi Bi Itika Mwangosi  .
Kutokana na hali hiyo zoezi hilo lilisogezwa  mbele na kupigwa  wimbo maarum wa  kumkumbuka Mwangosi na baada ya hapo Kibanda alikaribishwa  kukabidhiwa  tuzo yake.
Hata  hivyo Kibanda  alionyesha  kuwa na simanzi nzito na hata  kuueleza  umma uliokuwepo hapo kuwa tuzo hiyo inamtia majonzi zaidi kwa kukumbuka kifo  cha Mwangosi na yale  yaliyomkuta yeye kwa kuvamiwa na kutoborewa  jicho lake .
Hivyo alisema mbali ya kesio hiyo kuendelea  kuzunguswa bado yote anamwachia Mungu aliyemfanya kuwa hai hadi leo na kuwa katika fedha  alizopata  za tuzo  asilimia 10 atamrejeshia  mwenyezi Mungu na fedha inayobaki  atagawana  nusu kwa nusu na mjane wa Mwangosi
wakati huo  huo wanahabari  nchini  wametakiwa  kujenga  umoja katika  kupinga sheria  kandamizi  ya  vyombo  vya habari  na  wanahabari nchini inayatarajia  kupitishwa na  wabunge wa  bunge la jamhuri ya  muungano wa Tanzania.
Meneja  wa uthibiti  wa ubora  kutoka  baraza la habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa  kauli hiyo  leo  jijini Mwanza wakati  wa hafla  ya  kukabidhi tuzo  ya  kishujaa na uandishi  uliotukuka  ya  Daudi Mwangosi .
Mtambalike  amesema  kuwa  idadi ya  waandishi  kutekwa na kuuwawa  imezidi  kuongezeka  hapa nchini  huku kasi  ya  serikali  kuvifungia vyombo  vya habari  pia  inaendelea  kuongezeka .
Hivyo iwapo wanahabari  nchini  hawataungana  katika  kupinga  manyanyaso  dhidi  ya  vyombo vya habari na  kupinga  sheria  kandamizi  dhidi ya  vyombo  vya habari na wanahabari suala  la uhuru  wa  vyombo  vya habari nchini  litaendelea  kubaki ndoto.
Kwa  upande wake rais  wa umoja  wa  vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania  (UTPC) Keneth Simbaya alisema  kuwa tuzo  hiyo  inayotolewa ni  tuzo ya  kwanza  kutolewa nchini Tanzania  kwa  waandishi  wanaopata  matatizo wakati  wanatekeleza wajibu  wao.
Simbaya  alisema kuwa UTPC  imeamua  kuanzisha  tuzo  hiyo kama  njia ya  kuwapa  moyo  wanahabari na  kuuthibitishia umma kuwa  wanahabari  nchini  hawatakata tama katika  kutumikia tasnia  hiyo.
Alisema iwapo  jamii inapaswa  kujua ni vema  serikali  kukubali  kutoa habari kwa jamii inayopasa  kujua na  inayo haki ya  kupata  habari.
“ Serikali itambue  kuwa  inapohitaji  wananchi  kuchangia maendeleo ni vema itambue  kuwa  wananchi hao  wana haki ya kupata  taarifa  mbali mbali  ya kile  walichochangia….ndani  ya  tukio la mauwaji  ya  Mwangosi tumejifunza mambo mengi sana kwani tunapofanya kazi  zetu  wapo  wasiopenda  kuona  tunafanya kazi  zetu hiyo”
Pia  alisema  ni vizuri wananchi  kutambua  kuwa wakati  wanahabari nchini  wakitetea  kupata  habari wasifikiri  wanahabari  wanajipangani  wao  .
Kwani  alisema  kuwa  jitihada za  wanahabari  kupigania  uhuru  wa kupata  habari zinapaswa  kuungwa mkono na kila raia  wa Tanzania  ambayo ana haki ya  kupata  habari
Jaji mkuu  tuzo  hiyo Hamza Kasongo alisema  kuwa mchakato  wa kumpata  mshindi  ulifanyika kwa kipindi  cha miezi miwili kuanza septemba hadi Octoba mwaka  huu.
Tuzo   hiyo ya  uandishi  wa  habari wa  kishujaa na utumishi  uliotukuka  ya Daudi Mwangosi  imetolewa kwa  Absalom Kibanda mahariri  wa kampuni ya  new habari (2006) Ltd  na mwenyekiti  wa  jukwaa la  wahariri nchini (TEF)