Saturday, October 26, 2013

BREAKING NEWS:KUTOKANA NA HITLAFU YA UMEME ILIYOJITOKEZA SHOO YA FIESTA DAR KUENDELEA SAA 9 ALASIRI LEO... !!!


Wasanii J Martins kutoka nchini Nigeria na Ommy Dimpoz wa hapa nchini wakilishambulia jukwaa la Fiesta leo alfajiri kabla ya hitilafu ya umeme kutokea.
BAADA ya shoo ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 jijini Dar kusimama kwa muda leo alfajiri kwa hitilafu ya umeme, itandelea tena saa 9 alasiri leo katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam bila kiingilio.
Akizungumza na baadhi ya mashabiki wa tamasha hilo waliokuwepo viwanjani hapo baada ya hitilafu kurekebishwa, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alisema kuwa shoo itaendelea saa 9 na wasanii Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' Davido kutoka Nigeria, Mohombi kutoka Sweden, Nay wa Mitego na Bendi ya Twanga Pepeta watatoa burudani ya nguvu.
Aliongeza kuwa mashabiki wategemee 'sapraiz' kibao wakati wa shoo hiyo. Wasanii waliopiga shoo baada ya umeme kurudi katika hali yake ni pamoja na Kalapina, Chid Benz na Darasa japo mashabiki wengi walikuwa wameondoka viwanjani hapo.