Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye ndege,
baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma jioni hii, kwa ajili ya
kufunga semina ya mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za
wilaya na mikoa inayomalizika kesho.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete baada ya kuwasili mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, baada ya kuwasili Uwanja wa
Ndege wa Dodoma jioni hii
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye Uwanja wa Ndege mjini Dodoma
baada ya kuwasili jioni hii.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimwongoza Rais Kikwete kwenda eneo
la mapumziko baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Kulia ni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kumlaki, Uwanja wa Ndege wa Dodoma jioni hii.
--