Wednesday, October 30, 2013

ACTRESS CHUCHU HANS ATIMKIA INDIA KUONDOA STRESS BAADA YA KUKWAA SKENDO YA KUGOMBEA PENZI LA RAY.


 


Chuchu Hans ametimkia nchini India baada ya kukwaa skendo ya kugombania penzi la Vicent Kigosi(Ray) na muigizaji mwenzake Blandina Chagula(Johari). Inadaiwa kuwa tangu skendo hiyo iliporipotiwa magazetini na mitandaoni Chuchu ambaye ameigiza filamu nyingi mwaka huu amekuwa akiishi kwa kujifichaficha ili kukwepa macho ya watu baada ya msala huo na hivyo kuamua kwenda India kwa shangazi yake ili kuondoa stress na hata kuondoka kwake aliondoka kupitia Zanzibar na sio Dar es salaam ili kukwepa macho ya wanaomjua. Chanzo kilicho karibu na Chuchu kiliambia Globalpublishers "Amekwenda kwa shangazi yake India, amesafiri wikiendi hii kwa ndege ya Emirates, tena ili kukwepa macho ya watu ameondokea Zanzibar. Ile skendo imemchanganya sana"