Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk. Tzeba amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152 badala ya 500 zilizoanza kutozwa hapo jana.
Akiongea toka mkoani Dodoma, Tzeba ameweka wazi kuwa Waziri wa Fedha wa Rwanda aitwaye Gatete na wa waziri wa Uchukuzi wa Rwanda aitwaye Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152 iendelee kutumika.
Tzeba amedai kuwa ofisa mmoja katika Wizara ya Fedha ya Rwanda ndiye aliyekurupuka na kutangaza mabadiliko hayo kwa mdomo.
Waziri wa Fedha wa Rwanda alipoulizwa na mwenzake wa Tanzania, alishituka na kuahidi kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ambapo ndani ya muda mfupi jibu lilipatikana kuwa agizo la ofisa huyo wa Rwanda halikuwa halali.
Mbali na kauli ya Tzeba, habari za CHUMBANI ambazo mpekuzi wetu amezipata zinadai kwamba uamuzi huu umefikiwa na serikali ya Kagame baada ya Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kupunguza ushuru wa barabara ( Road Toll) kwa magari yenye plate numbers za Rwanda kwa asilimia 170.
Kwa hali hii, ni dhahiri kuwa huu utakuwa ni ushindi mkubwa kwa Rwanda ikizingatiwa kuwa umbali kutoka Dar es Salaam mpaka Rusumo ( mpakani )sio sawa na umbali kutoka Rusumo mpaka Kigali.