Katika
eneo la tukio la mauaji hayo mlango wa nyumba ulikuwa umefungwa kwa
nje, na mara baada ya kufunguliwa maiti ya baba wa familia hiyo Jonus
Elias (44) ilikuwa sebuleni huku ikiwa imechinjwa, nako chumbani
kulikuwa na mwili wa mama wa familia hiyo Bi. Lucia Jonus na mwili wa
mtoto aliyekuwa na umri wa miezi saba.
Polisi wakishirikiana kupakia miili ya marehemu hao kwaajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Watu watatu wa familia moja
wameuawa kikatili usiku wa kuamkia jana na watu wanaosadikika kuwa ni
majambazi katika kijiji cha Ihila B, Kata ya Buhongwa Wilaya ya
Nyamagana hapa Mkoani Mwanza.
Taarifa za awali kutoka eneo
la tukio zinaeleza kwamba watu hao ambao ni Jonus Elius (44) ambae ni
baba wa familia, Lucia Jonus (35) ambae ni mama wa familia pamoja na
Eliud Jonus (1) ambae ni mtoto wa familia hiyo wameuawa kikatili
kufuatia baba wa familia hiyo kuchinjwa shingoni na kitu kinachosadikiwa
kuwa na ncha kali huku mama na mtoto wakisadikiwa kunyongwa na kitu
kinachosadikiwa kuwa ni waya.
Uchunguzi wa awali unaeleza
kwamba kulikuwa na mgeni ambae alifika katika familia hiyo ndani ya siku
nne kwa ajili ya shughuli ya kufyatua tofali za ujezi wa nyumba ya
familia hiyo, ambae anasadikiwa kutenda tukio hilo kwa kuwa baada ya
mauaji hayo ametoweka katika familia hiyo.
Akiwa katika eneo la tukio
Mkuu wa makosa ya upepelezi Mkoa wa Mwanza RCO Joseph Konyo ameeleza
kwamba mauaji hayo yanasadikika kutekelezwa kati ya majira ya saa nane
hadi saa kumi usiku wa kuamkia leo.
Aidha RCO Konyo amesema kwamba
bado uchunguzi zaidi juu ya mauaji hayo unaendelea na taarifa zaidi
zitatolewa na msemaji wa jeshi la polisi Mkoa wa wa Mwanza ambae ni RPC
pindi upelelezi utakapokamilika ambapo amewataka wananchi kutoa
ushirikiano wao ili kuweza kufanikisha upelelezi huo mapema.
Kufuatia mauaji hayo ya
kusikitisha ambayo yanasadikika kutekelezwa huku sababu zikiwa bado ni
kitendawili, wananchi na majirani wa eneo hilo la tukio wameeleza
kusikitishwa kwao na matukio ya aina hiyo ambayo wametoa rai kwa jeshi
la polisi kuhakikisha likamilisha upelelezi wake mapema na kuhakikisha
kwamba wahusika wote wanafikishwa katika vyombo vya dola