Saturday, August 17, 2013

YALIYO JILI KWENYE UZINDUZI WA VIDEO YA YAHAYA @NYUMBANI LONGUE

Burudani nzima ilianza mida ya saa nne na nusu usiku ambapo Machozi Band iliporomosha ngoma juu ya ngoma pasi na kuwa na Binti machozi alias Anaconda, Lady jay dee ambaye alikuwa  Kenya alipokwenda kuchukua video yake hiyo.
Huku watu wakiendelea kuongezeka kadri muda ulivyosogea ndipo shangwe kubwa zilipoibuka mida ya saa sita kasoro usiku pale mgeni rasmi BBA the chase Fezza Kessy alipotangazwa kuingia ukumbini.

Show iliendelea kwa Machozi Band kudondosha ngoma kali kisha Fezza alipewa nafasi ya kusalimia watu kabla ya kuitwa tena jukwaani kula keki iliyoandaliwa na shabiki wa Machozi Band.


Shangwe zilikuwa za kushiba zaidi mida ya saa saba za usiku baada ya Anaconda- Lady jay dee kupanda jukwaani na kugonga ngoma mchanganyiko kabla ya kumualika tena Fezza jukwaani ambaye alitoa thanks nyingi kwa Jide bila kuimba.

kila kitu jukwaani kiliwekwa chini na macho yote yakahama kutoka jukwaani kuzielekea projectors zilizopo ndani kucheki kichupa hicho.


Yahaya video ni kali na ina kila sababu kufanyiwa Lounging ya dizain ile. Kama ulimis, umekosa uhondo

Much respect to Machozi Band, Nyumbani Longue management, Lady jay dee, Team Anaconda na wote waliosababisha kitu hii kufanyika.