Thursday, August 8, 2013

Wanafunzi Ilboru wapo kwenye mgomo mkali

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Phillipo Mulugo
Mgomo wa wanafunzi wa Sekondari ya Ilboru, iliyopo wilayani Arumeru, kutoingia madarasani uliingia siku ya pili jana, wakishinikiza mwanafunzi mwenzao Ibrahim Kaebo wa kidato cha tatu ‘C’ aliyefukuzwa na bodi bila kupewa nafasi ya kujitetea, kurejeshwa shuleni.


Akizungumza mjini hapa, alisema yeye ni Makamu Mwenyekiti wa chakula na bwalo, hivyo akiwa kiongozi alikuwa anakabiliwa na changamoto za chakula kuwa kibovu na wenzake kugoma kula, hivyo kama wajibu wake aliandika taarifa, jambo lililomponza kuwa anajifanya mjuaji.

Alisema alimsindikiza mwanafunzi mwenzao hospitalini, (hakumtaja jina), baada ya kuumizwa mkono kwa kuchapwa viboko na mwalimu, jambo lililopelekwa k