Friday, August 16, 2013

WAISLAMU WAHIMIZWA KUJA KUSALI KWA WINGI, MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI JIJINI DAR NA KUTOOGOPA ASKARI

Jeshi la polisi nchini limeshaweka ulinzi wa kutosha katika msikiti wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia choko choko za maandamano zilizopangwa kufanyika baada ya sara ya Ijumaa.
Kwa mujibu wa kamera ya E.S.L  Blog iliyoweka kambi eneo la tukio, mpaka sasa gari tatu za polisi zimeshawasili eneo la msikiti huo kuimarisha ulinzi.

"Ndugu zangu msiogope kuja kusali leo ni jihadi, udhalilishaji wa serikali ya CCM... LEO NI JIHADI. Msiogope kujakusali maana tumeshavipigia vyombo vyote vya habari wakiwemo TBC 1, Channel 10, ITV na waandishinwote watakuwepo kuona hichi walichopanga kukifanya hawa. Hayo ni maneno ambayo yanatangazwa kwa sasa na kiongozi mmoja wa msikiti huu.

Mara baada ya maneno haya naona magari ya askari yaliyokuwa yamepaki kwenye mlango wa msikiti huo yameomdoka na kupaki pembezoni.

Ila mpaka sasa hali ya usalama ni nzuri japo kumekuwa na choko choko za kufanyika maadamano jambo ambalo linatia hofu wakati wa maeneo haya ambao wameanza kufunga maduka yao.

Endelea kufuatilia mpaka mwisho wa sakata hili.