Sisi, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay – atul Ulamaa),
tumepokea kwa masikitiko makubwa habari za kushambuliwa na kujeruhiwa
kwa silaha za moto, Sheikh Ponda Isa Ponda, huko Morogoro, Jumamosi
Agosti 10, 2013.
Tunalaani vikali kitendo hicho na tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuchukua hatua kali na za haraka dhidi ya wale wote
walio husika katika tukio hili lenye kuumiza nyoyo za wengi.
Aidha tunawasihi Waislamu na jamii kwa ujumla kuwa watulivu, wenye
subira na wenye kunyenyekea kwa Mola wao katika jambo hili zito, wakati
tunasubiri vyombo vya dola vichukue hatua zinazo stahiki dhidi ya
wahusika wa tukio hili.
Tunamuombea Sheikh Ponda Isa Ponda Allah Amponye haraka na Am,pe baraka katika umri wake. Amin
Sheikh Suleiman Amran Kilemile
Mwenyekiti
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania