Tuesday, August 13, 2013

SIFURAHISHWI NA MATUMIZI YA PICHA ZANGU" RAYUU


Rayuu mwigizaji wa filamu Swahilihood.
MWIGIZAJI wa filamu wa kike Alice Bagenzi ‘Rayuu’ anashangazwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia picha zake na kuandika wanavyojua bila hata ya ridhaa yake huku akidai kuwa aliwahi kuelezea mazingira ya picha hizo zilifikaje katika mitandao ya kijamii, Rayuu anatabika na picha zake alizowahi kupiga akiwa nusu uchi na kuanikwa katika mitandao.

.
Alice BagenziRayuu akiwa katika pozi
Alice BagenziRayuu akiwa katulia.
Alice BagenziRayuu msanii wa filamu Bongo.
“Nashanga kuona kuna watu ambao wanajichukulia maamuzi ya kutumia vibaya picha zangu katika mitandao ya kijamii bila ridhaa yangu, si kitu ambacho kinanifurahisha lakini sina jinsi na niliwahi kuwaambia na kukiri kuwa zile picha nilizipiga kwa kutumia simu yangu na bahati mbaya kuna mtu akazitumia vibaya, nilihitaji kuziondoa lakini tayari kuna wengine walizihifadhi na ndio wananisumbua nazo,”
Rayuu kwa sehemu moja anajutia ukuaji wa teknorojia hasa mitandao ya kijamii kwani pengine anaamini kuwa laiti kama ingelikuwa ni gazeti na si mitandao pengine tukio lake lisingeendelea kuongelewa au picha zake hizo baadhi ya watu kuweka katika akaunti zao za facebook, msanii awali aliona kama ni tukio la kupita lakini ni kitu ambacho kimekuwa kikipotea na kurudi, anawaomba watu wasitumie picha zinamchafua bila sababu ya msingi.