Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam tayari kwa uzinduzi wa filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti wake Jonson Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla
Lulu akilakiwa kwa mbwembwe na vijana walioandaliwa kwa kazi hiyo
Muigizaji wa filamu Jacob Steven akizungumza na wageni wa kampuni ya Proin Promotion katika uzinduzi huo
Jonson Lukaza akizungumza na baadhi ya wageni wake waliohudhuria katika uzinduzi wa filamu hiyo
Muigizaji Vicent Kigosi Ray akiwasili katika uzinduzi huo unaofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City
Mwenyekiti wa kampuni ya Proin Promotion Bw. Jonson Lukaza katikati akizungumza na baadhi ya waigizaji wa filamu Rich Rich na mwenzake
Katikati ni Mama Mzazi wa Elizabeth Michael akiongea kwa furaha huku akitoa machozi na Msanii wa Filamu Tanzania Wema Abraham Sepetu(kushoto) na Rafiki yao katika Uzinduzi wa Filamu ya Lulu ulioandaliwa na kufanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
Wema Sepetu (aliyepiga magoti) akikumbatiana na Mama yake mzazi Lulu wakati wa Uzinduzi wa Filamu ya Mwanae Elizabeth Michael katika Ukumbi wa Mlimani City, uzinduzi uliokwenda sambamba na burudani kutoka Kwa Wasanii mbalimbali wa Muziki wa Bongo Fleva katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo.
Wadau wakisakata Mduara katika uzinduzi huo wa filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa kuamkia leo, Uzinduzi huo wa Kufa mtu uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ulifana kupita Kiasi