Saturday, August 3, 2013

MWANAMKE MWINGINE WA KITANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ZIMBABWE!!




Mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 34, wiki iliyopita alikamatwa katika kiwanja cha kimataifa cha  Harare baada ya kukutwa na dawa haramu zenye thamani ya dola 45,000 kwa bei za mtaani alipowasili kutoka India.
MWANDISHI MWANDAMIZI
 Jackline Mollel Richard, ambaye anaishi Afrika Kusini, hakuambiwa ajitetee alipokuwa mbele ya hakimu wa Harare Donald, Ndirowei . Aliwekwa rumande chini ya ulinzi hadi Julai 27
Jackline amekutwa na milki ya kilo 15 ya efedrini ambayo  inasaidia kushitua mfumo wa moyo na mfumo wa  neva. Ni mara nyingi hupatikana katika dawa za mitishamba na chakula.
Inasemekana kuwa  Jackline aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare na ndege ya Emirates kutoka India . Alitoa passport yake katika meza ya uhamiaji na ndipo afisa tahadhari alipowatonya wapelelezi wa madawa ya kulevya kwamba mama huyo ana viza ya India ambayo ni chanzo maalumu kwa ajili ya madawa haramu.
mahakama ilipata taarifa kuwa Jackline alichukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa na wakati anakaguliwa na wapelelezi hao alikutwa na bahasha 30 za khaki ikiwa na vitu vyeupe ambayo vilikuwa vimefungwa pamoja na  kitambaa ndani ya beg la maruni.
Vipimo vilifanyika kwenye bahasha hizo na ikabainika kuwa ilikuwa efedrini. Madawa ya kulevya hayo yalichukuliwa  kwa ajili ya kurekodiwa na kupima  uzito