Mubarak kuachiwa huru kwa dhamana
Hosni Mubarak
Mahakama nchini Misri inatarajia kutoa uamuzi wa ama kumuachia huru kwa dhamana au la, Rais wa zamani nchi hiyo Hosni Mubarak.
Bwana Mubarak anakabiliwa na mashtaka ya rushwa ambayo yamemfanya asalie rumande bila dhamana.
Wakati
huo huo, Mawaziri wa mambo ya nje na masuala ya kigeni wa nchi za umoja
wa Ulaya wanakutana kujadili hatima ya Misri, huku wengine watarajia
kufuta kabisa misaada yote kwa taifa hilo lililopo kwenye hali tata kwa
sasa.Rais huyo wa zamani wa Misri mwenye umri wa miaka 85 pia anakabili
kesi nyingine ya kushirikiana katika mauji ya waandamanaji wakati wa
vuguvugu la mapinduzi ya kiraia yaliyomuondoa madarakani mwaka 2011.
Baadhi ya
mawaziri wameomba fungu la msaada wa Yuro bilioni 5 sawa na dola
Bilioni 6.7 wanalopewa Misri kufutwa baada ya watu zaidi ya 900 kuuwawa
kwenye ghasia tangu wiki iliyopita.
Vifo
hivyo vimetokea mara baada ya serikali ya mpito kuamuru vikosi vya
polisi na jeshi kufunga kambi mbili za wafuasi wa rais aliyeondolewa
madarakani Mohamed Morsi.
Vyanzo
vya habari vya mwandishi wa BBC mjini Brussels, Matthew Price vinasema
mawaziri hao wanakusudia kusitisha misaada ya kijeshi na usalama
inayotolewa na nchi mbalimbali za ulaya kwa taifa la Misri.
Mkurugenzi
wa sera kwenye umoja wa Ulaya,Baroness Catherine Ashton ameomba kufanya
suluhisho la kisiasa nchini Misri na ana imani ya kujenga matumaini ya
kufanyika hilo baina ya serikali ya mpito na chama cha Muslim
Brotherhood.
Nako
nchini Marekani maofisa wakuu wa serikali ya Obama wamekuwa katika
mkutano wa dharura mjini Washington kujadili iwapo waendelee kutoa
msaada wa dola bilioni 1.3 kwa serikali ya Misri.
Mamia ya
wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood wameuawa ndani ya wiki moja na
Marekani imeonya kuwa kukosa kuijumuisha Muslim Brotherhood katika
suluhisho la kisiasa la nchi hiyo, kutaathiri msaada unaotolewa, ambao
mwingi unaenda kwa jeshi.
UCHELEWESHWAJI UNATARAJIWA
Bwana
Mubarak 85,alishitakiwa mwezi Juni mwaka 2012 kwa mashtaka ya kuhusika
na mauaji ya waandamanaji mwaka 2011 na kufungwa kifungo cha maisha
jela.
Lakini mwezi Januari 2013 alishinda rufaa aliyokata na mahakama ya rufaa kuamuru kesi yake isikilizwe upya.
Kesi hiyo
ilianza upya mwezi Mei 2013,lakini bwana Mubarak tayari amekwishakaa
kizuizini kupita muda ambao unatakiwa kwa mashtaka hayo.
Wakili wa
Mubarak , Fareed Al Dib amesema anatarajia mteja wake ataachiliwa huru
baada ya amri ya mahakama na atasalia na kesi za mashitaka dhidi ya
rushwa pekee.
Licha ya
upande wa mashitaka kutarajiwa kupinga kwa kukata rufaa dhidi ya
kuachiwa kwake,jambo ambalo litachelewesha kutoka kwake gerezani.
Kesi hiyo pia inahusiana na tuhuma za rais huyo kupokea hongo kama zawadi kutoka kwa gazeti la serikali Al-Ahram.
Mwandishi
wa BBC mjini Cairo anasema familia ya Mubarak imelipa gharama zote na
zawadi ambazo anadaiwa kuzichukua, suala ambalo linamuongezea matumaini
wakili wake kuwa huenda mteja wake akaachiliwa huru.
Hukumu ya rufaa itasomwa kwenye gereza ambalo Mubaraq amefungwa.
Wadadisi
wanasema iwapo Mubarak ataachiliwa, hiyo itarudisha hisia za wengi za
kwamba jeshi linataka kurejesha utawala ambao uliondolewa kwa mapinduzi
ya kiraia ya mwaka 2011,
Suala ambalo huenda likarudisha maandamano makubwa na ghasia zaidi kuendelea kuzuka nchini humo