Mtu
aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela
nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya
heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).
Shirika
la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013
limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa
jina la Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege
cha LAX mjini Los Angeles akitokea Nairobi.
Mackubi
alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court) jijini LA na
kusomewa mashitaka siku ya Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri
kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya
kazi.
Inaripotiwa
kuwa maafisa waligundua uzito usio wa kawaida wa laptop aliyokuwa nayo
Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana walipompekua. Walipompeleka kumpekua kwa
mara ya pili kwa kina zaidi, walijaribu kuwasha komyputa hiyo bila
mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina alama za kufunguliwa awali
(tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa ndani ambapo walikuta
gramu 800 za heroin zimefichwa.
Mackubi
alisema alikuwa akutane na mwanamke anayeishi jimboni Alabama, ambaye
walifahamiana kwenye mtandao wa internet. Maafisa wamesema kuwa
Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa LAX wakisafirisha dawa za
kulevya kwa njia hiyo.
Hukumu impasayo Mackubi imepangwa kutolewa tarehe 11 Septemba.