Friday, August 30, 2013

MSAKO MKALI WAENDELEA KUBAINI VIBANDA VINAVYOONYESHA MIKANDA YA NGONO DAR

MSAKO mkali unaendelea kuvifumua vibanda vya video vinavyokiuka maadili kwa kuonesha mikanda ya ngono ‘X’ kwa watoto.
Baadhi ya DVD za ngono zilizonaswa.
Tukio la hivi karibuni limetokea Tandale Uzuri jijini Dar ambapo vijana wawili, Yasini Issa (25) na Kivuluga Abdi (27) wametiwa mbaroni kutokana na kudaiwa kuendesha biashara hiyo haramu.
Kabla ya tukio hilo, baadhi ya wazazi wanaoishi eneo hilo walipiga simu katika ofisi za gazeti hili wakilalamikia matukio hayo ya watoto kuoneshwa mikanda hiyo inayokiuka maadili ya Kitanzania.
Mmoja wa watuhumiwa akiandaa mitambo kwa ajili ya kuonyesha picha hizo za ngono.
Baada ya kupata ukweli wa tukio hilo, Jumatatu iliyopita waandishi wetu kwa kutumia kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), waliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Magomeni na kujipanga  kufanikisha zoezi la kuwatia mbaroni wahusika.
Upelelezi wa OFM uligundua kuwa kibanda hicho kilikuwa kikianza kuonesha mikanda hiyo michafu kuanzia saa mbili za usiku na kuendelea.  
Ukumbi wa kuonyesha video za ngono.
Mmoja wa wandishi wetu alijifanya mteja wa kuangalia sinema katika kibanda hicho na kulazimika kuingia katika kibanda hicho kwa kulipa shilingi 400.
Akiwa ndani ya kibanda hicho, aligundua kuwepo kwa watu wa jinsi tofauti na watoto wakiendelea kuangalia sinema mbalimbali zilizokuwa zikioneshwa.
Baadhi ya matangazo ya video za ngono.
Mwandishi huyo alikuwa akiwasiliana na mwenzake aliyekuwa nje ya kibanda cha video pamoja na askari wa Kituo cha Magomeni.
Ilipotimu saa mbili kamili, picha zilizokuwa zikioneshwa ndani ya kibanda hicho zilibadilishwa na kuwekwa CD za X huku watoto wakiwa wamejaa ndani.
Mtuhumiwa mwingine akipanda difenda kuelekea kituo cha polisi.
Mwandishi wetu aliwafahamisha askari kwamba mchezo ulikuwa umeshaanza nao wakafika na kukuta tukio hilo likiendelea huku watu waliojazana ndani ya kibanda hicho wakikimbia na kuwaacha wahusika waliotiwa nguvuni.
Baada ya askari kufanya ukaguzi ndani ya jengo hilo  walizikuta kondomu zilizokuwa zimeshatumika ambazo inadaiwa baada ya watu kuangalia picha hizo walikuwa na tabia za kufanya ngono ndani ya kibanda hicho.
Watuhumiwa hawa hapa.
Mwisho, watuhumiwa walibebeshwa vitendea kazi vyao na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Magomeni na kufunguliwa kesi ya KUONESHA PICHA ZA NGONO yenye kumbukumbu namba MAG/RB/9722/2013. 

SOURCE:GPL