Meneja
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akizungumza na
waandishi wa habari ambapo amewashukuru wateja wote DStv na Watanzania
walioshiriki katika kumpigia kura mshiriki aliyeiwakilisha Tanzania
kwenye shindano la Big Brother The Chase Season 8 Feza Kessy ambaye
alibakiza siku chache tu kuweza kufuzu 14 mpaka kumalizika kwa shindano
hilo. Barbara Kambogi ameowaomba wateja wa DStv waendelea na Watanzania
kwa ujumla isiwe mwisho wa kutazama mchezo huo kwa sababu mshiriki wa
Tanzania. Katikati ni Mshiriki wa Tanzania kwenye shindano la Big
Brother The Chase Feza Kessy na Kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya simu
za mkononi Airtel Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano
hilo.