Picha na Maktaba
Nyumba
6 zimechomwa moto katika Kijiji cha VODA ,Tarafa ya Mbwewe Mkoani
Pwani,baada ya wanakijiji kuvamia gari la mizigo lililokuwa limebeba
mitumba kuanguka na kufunga barabara ambapo wakazi hao walianza kupora
hali iliyosababisha wenye mizigo kuingia kijijini kuwasaka waliopora
mizigo hiyo.
Kamanda
wa usalama barabarani Chalinze Afande Sule amesema sehemu ya barabara
hiyo ya Chalinze-Segera imefungwa na kusababisha abiria kutoka Dar Es
Salaam kwenda tanga,Kilimanjaro na Arusha kukwama.Chanzo itv