Mkunga huyo akionyesha mkeka unaotumika kuwatandikia wajawazito wanaokuja kujifungulia katika kliniki yake
Mkunga
akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa
ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.
Mwanamke
mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK mwenye umri wa miaka
ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya ,amejifungua mtoto jinsi ya
kiume na wakati huohuo na chura.
Mkunga
aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa MBUYUNI wilaya ya chunya
amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti 13 mwaka
huu,mara mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe aitwaye
BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye umri wa miaka thelathini na tano
MATRIDA
amesema huo ni uzao wake wanne na kwamba alishangazwa na kiumbe hicho
ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo lolote na pia alifurahia
kupata mtoto wa kiume mwenye afya na alisikitishwa kupata hicho kiumbe
ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye vidole vinne na miguu ya nyuma
vidole vitano vya binadamu.
Kwa
upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa katika kondo lake na chura
alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na pia
ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza mwanamke
alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa
tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu kwa hiyo hili
ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.
Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada
ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha MBUYUNI bwana
CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji MICHAEL SANZIMWA
ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo kuondoa kiumbe
hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.
Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
|