Saturday, August 31, 2013

BREAKING NEWS:MOTO WAWAKA KARIBU NA JENGO LA BANK YA UBL MKWEPU POSTA.

Moto umeripotiwa alfajiri ya kuamkia Jumapili ya leo katika jingo moja lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwenye mtaa wa Samora na Mkwepu Street.

Kikosi cha Polisi kilifika mapema baada ya kupokea taarifa hizo na kisha kikosi cha zimamoto kilifika kikiwa na huduma moja tu ya gari la maji ya kusaidia kuzima moto huo.

Juhudi hizo ambazo kwa hakika hazikukidhi haja, zililazimu kuomba usaidizi wa kikosi cha zimamoto cha kampuni binafsi ya Knight Support.

Hadi taarifa hii inachapishwa (alfajiri ya saa kumi) juhudi za kuuzima kabisa moto huo zilikuwa bado zikiendelea.

Nimapema sana kufahamu chanzo na hasara iliyosababishwa na moto huo.

Taarifa zaidi zitatolewa na vyombo na mamlaka husika.