Friday, August 2, 2013

Batuli awataka Flora Mvungi na H.Baba wasiwe ‘wanafiki’

Muigizaji mrembo wa filamu nchini, Yobnesh Yussuph maarufu kama Batuli amepingana na kauli iliyotolewa na wanandoa wenye miezi mitatu sasa, Hamis Baba aka H.Baba na Flora Mvungi.

Hamis na Flora siku wakifunga ndoa

Mastaa hao hivi karibuni kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, walidai kuwa industry ya filamu Tanzania imejaa ‘manisnitch’ kibao ndio maana hawakupata support ya kutosha kwenye harusi yao.

Batuli aliamua kujibu shutuma hizi kwa niaba ya waigizaji wengine wa filamu.

“Flora Mvungi usitulaimu usituite wanafiki ni neno baya sana, tumewachangia wangapi? Kwanini wewe tusikuchangie? Ulialika uwatakao usilalamike,” alitweet Batuli.
Batuli

“Mr & Mrs H Baba napinga kauli ya kusema ndoa sio mpaka ualikwe jamani hivi kweli kabisa nivae gauni langu niende ukumbini sijaalikwa?” aliongeza.

Kwenye kipindi hicho, Flora alidai kuwa harusi yao ilihudhuriwa na watu wachache aliowaalika lakini alidai kuwa hata wale ambao hawakupata mialiko wangeweza kuhudhuria.