leo katika kongamano la kuita umoja wa kiislamu katika yanayowakabili waislamu mkoani morogoro.kongamano lilienda vizuri likiwa limepambwa na masheikh wakubwa wakubwa kama vile Riko, mwaipopo,kondo na sheikh ponda.sheikh ponda alikuwa wa mwisho kutoa mawaidha na aliaga waislamu ili aweze kuelekea katika msikiti wa mungu mmoja hivyo waislamu walitaka kumsindikiza sheikh ponda mpaka msikiti wa mungu mmoja.maaskari waliovalia nguo za fildforce wakiwa kwenye defender waliingia na kuanza kulifuata gari kwa nyuma.waislamu waliendelea kulizunguka gari la sheikh ponda ila maaskari walianza kupiga mabomu ya machozi ili kutawanya wananchi kisha kuifukuza gari la sheikh ponda