Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la mlipuko nje ya msikiti wa Sunni uliopo jijini Tripoli, Lebanon.
(PICHA ZOTE NA AP)
MILIPUKO mikubwa miwili imetokea leo nje ya misikiti katika jiji la Tripoli lililopo Kaskazini mwa Lebanon jirani na Syria. Katika milipuko hiyo, watu 27 wanadaiwa kupoteza maisha, wakati 350 wakijeruhiwa. Milipuko hii imeongeza mvutano nchini Lebanon ikiwa ni matokeo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Syria kati ya wafuasi na wapinzani wa utawala wa Rais wa Syria, Bashar Assad.