Monday, July 29, 2013

Waziri Mkuu wa Thailand atarajiwa kuwasili Tanzania kesho kwa ziara ya kikazi na pia kutembelea mbuga za wanyama.


DV1308102
 Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra atawasili kesho 30 Julai, 2013 majira ya saa 6.30 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J.K. Nyerere na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Usiku atashiriki katika dhifa maalumu ya Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake.