MAZISHI ya mama mzazi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ally Mohamed 'Z-Anto', Bi. Abilai yalifanyika jana jioni katika makaburi ya Tungi-Shuleni yaliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Marehemu Bi. Abilai alifariki Julai 9 mwaka huu saa nane mchana katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua kansa ya ini. Mamia ya waombolezaji waliungana na Z- Anto katika kumsindika mpendwa mama yake. Mtandao huu unatoa pole kwa familia nzima ya marehemu.
Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu. Amen!
source: globalpublishers