Wednesday, July 31, 2013

"SIJUTII KUTIMULIWA BIG BROTHER, NAAMINI HAIKUWA RIZIKI YANGU"...NANDO

Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando amesema hana majuto yoyote  baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo.

Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja  sheria za shindano hilo ,  leo amefunguka  kwa  mara  ya  kwanza ndani  ya  kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“I live my life with no regrets,”alisema Nando  na  kuongeza:

“Sitaki kufikiria  matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea...

"Najipanga upya ili  niendelee na maisha mengine. Vingapi vizuri  vimetokea nyuma ? 

"Tokea  nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace , nashukuru kwamba mmenipokea vizuri. 

"Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.”