Wednesday, July 31, 2013

SHEIKH PONDA ISSA PONDA APENDEKEZWA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015...


Ikiwa  imebakia  miaka  miwili  kabla  ya  kufanyika  kwa  uchaguzi  mkuu wa  Rais  na  wabunge  hapa  nchini,baadhi  ya  waumini  wa  kiislamu  wameanza  kupendekeza  wagombea  wa  urais  wanaoona  kuwa wanafaa  ambapo  jina  la Sheikh  Ponda Issa Ponda  limeongoza....

Mapendekezo  hayo  yamedhihirika   katika  mihadhara kadhaa  anayoifanya Ponda  katika  mikoa  mbalimbali  nchini,ambako  amekuwa  akipendekezwa  na  kushauriwa  na  waumini  agombee  nafasi hiyo.....

Walianza  waumini  wa  msikiti  mkuu  wa  Ijumaa  wa  Arusha  alipokuwa  kwenye  ziara  mkoani  humo  ambapo  muumini  mmoja  alisimama  na  kusema  kwamba  kwa  mawazo  yake  anaona  Ponda  anafaa  kugombea  nafasi  ya  urais  kwa  vile  anaamini  kuwa  uwezo  wa   kuongoza  anao..

Alisema  mbali  na  uwezo pia  yuko  makini  katika  kusimamia  jambo lolote  lenya  maslahi  kwa  waislam  na  kwamba  mtu  wa  namna  hiyo  atafanya  vyema  zaidi  akipewa  dhamana  ya  kuongoza  nchi....

Inaelezwa  kuwa Ponda  alipotembelea  Zanzibar  alipata  wakati  mgumu  wa  kuwakataa  waislam  waliojitokeza   kumlaki  katika  misikiti  ya  Mpendae na  Mbuyuni  ambako  alifanya  mihadhara  na  kupendekezwa kugombea  urais  kwa  kura  nyingi  na  waumini  ....

Kufuatia  kusikika  kwa  mapendekezo  hayo,Kisiwa  lilimtafuta  Ponda  ili  kusikia  maoni  yake  juu  ya  maombi  ya  waislam  kumtaka  agombee  urais.

"Sikuwa  na  fikra  hiyo  hata  mara  moja,lakini  maadam limeletwa  nami  ni  kiongozi  wa  taasisi  ninawashukuru  waliofikiria  hivyo...

"Kwa  sasa  siwezi  kuzungumza  lolote  kuhusu  hilo, ntalifikisha  katika  taasisi  na  maulana  ndio  watakaolitazama  na  kutoa  uamuzi." Alisema  Sheikh Ponda

Ponda  alisema  kuwa  inawezekana  waumini  wakawa  na  mtazamo  huo  lakini  viongozi  wakawa  na  mtazamo  tofauti  kabisa,hivyo  akawataka  waumini  kuwa  na   subira  katika  hilo.