Monday, July 29, 2013

PICHA NA VIDEO JINSI NANDO ALIVYOTOLEWA NADNI YA JUMBA LA BIG BROTHER...!!

 5
Channel 197 & 198 za DSTV zimeendelea kutoa huduma ya kutazama bure washiriki wa Afrika wanaozifukuzia dola laki moja za shindano la Big Brother Afrika 2013 The Chase ambapo Tanzania ilikua ikiwakilishwa na Nando pamoja na Feza Kessy.


Saa tano usiku wa July 28 2013 zikiwa zimepita dakika kadhaa tangu Annabel wa Kenya na Sulu wa Zambia kutolewa kwenye eviction ya kawaida kila jumapili, Nando amekua Mtanzania wa kwanza kutolewa kwenye jumba la BBA Johannesburg South Africa 2013 baada ya ugomvi wake na mshiriki Elikem wa Ghana.


Ni ugomvi ambao ulitokea Ijumaa kwa wawili hao kutukanana matusi mpaka yaliyowajumlishia na wazazi ndani yake ambapo Nando alivuka mipaka ya sheria za BBA hivyo kuitwa kwenye Diary Room na kuonyeshwa video ya kilichotokea na dakika kadhaa baadae akatolewa BBA akiwa hapohapo Diary Room, hakuruhusiwa kurudi kuwaaga washiriki wenzake.


Hizi picha na video ambayo iko chini kabisa ni mfululizo wa matukio mbalimbali muda mfupi tu baada ya Nando kutolewa BBA.


1


Bimp wa Ethiopia alikua mshkaji sana wa Nando, hapa alikua na huzuni baada ya Nando kutolewa.2 

Hii picha hapa juu ni wakati Nando yuko Diary Room akionyeshwa video ya wakati wa ugomvi wake na Elikem na matusi aliyokua akiyaporomosha.


Hasira za Nando zilipitiliza mpaka kudiriki kusema mtu kama Elikem anastahili kufa ambapo pia baadae Nando alikutwa akiwa amelala na mkasi chini ya kitanda chake ikiwa sio mara ya kwanza kukutwa na silaha ndani ya BBA house, jamaa amekua na wiki 9 za historia kwenye The Chase.


Mwezi uliopita Nando alipewa onyo na Biggie baada ya kuvunja sheria kwa kuonekana akiwa na kisu kwenye party ya Channel O.4


3


6


Feza na ‘shemeji’ muda mfupi tu baada ya Nando kutolewa.7


8


9 

Baada ya Nando kutolewa Feza alinyanyuka na kwenda kukaa na Bimp wa Ethiopia, mshkaji wa Nando ambae alionekana kuwa na huzuni.




11 

Hii sio mara ya kwanza kwa Mtanzania kutolewa BBA kwa kuvunja sheria, mwaka 2011 Lotus alitolewa baada ya ugomvi wake na Luclay kuvuka mipaka na kupelekea Mtangazaji huyu kuvunja sheria za BBA.