Monalisa ni picha ndogo ya mwanamke ambayo ilichorwa na mwanasayansi na mchoraji wa kii
taliano aitwaye LEONARDO DA VINC. Picha hii inatambulika kama
miongoni mwa picha bora inayofahamika , kutembelewa na watu wengi na kuandikwa katika vitabu vya waandishi na
halkadhalika inayotoa maswal I mengi
mpaka sasa ulimwenguni. Inaaminika kwa wana theory kuwa ni picha ya mwanamke aitwaye LISA GERADHIN mke wa FRANSESACO GIOCONDO kwa sababu da vinc hakuweza kutoa maelezo
yoyote juu ya hii picha mpaka anakufa na pia inaaminika kuwa ilichorwa kwa oil
katika miaka ya 1503 mpaka 1506 ,picha hii ilichukuliwa na mfalme FRANCIS I of
france na mpaka sasa ni mali ya jamuhuri ya watu wa ufaransa .
NI NANI LEONARDO DA VINC
-
Kwa kumsikia Leonardo da vinc alikuwa ni scientist,
zoologist, mgunduzi (inventor ) na pia alikuwa ni genius. Miongoni mwa vitu
alivyovigundua leornardo da vinc ni pamoja na
·
Vifaa vinavyoweza kutumiwa na binadamu kupaa
·
Aligundua kuwepo kwa mafuta ndani ya mwili wa binadamu
·
Aligundua vifaa vya wazimiaji wa baharini(diving
suit)
·
Aligundua helkopta
·
Vifaa vya hatari vya kuua katika vita
Na
mambo mengine mengi aligundua, kazi nyingine aliyechora leornardo da vinc ni
ile ya LAST SUPPER. Da vinc alitumia si chini ya miaka 4 kuikamilisha picha ya
monalisa na hakuweza kutaja mpaka anakufa nini hasa monalisa?, yukowap?,na ina
maana gani ambayo imebua maswali mengi katika dunia ya sasa. Ilipofika mnamo
mwaka 1911 picha hii iliweza kuibiwa katika makumbusho ya ufaransa na
ikarudishwa baada ya miaka 2
KWANINI TUNAICHAMBUA PICHA HII
Ina
aaminika ulimwenguni kote kipaji alichokuwa nacho LEONARDO DA VINC kilikuwa si
cha kawaida na inasemekana yeye ndio alikuwa mwanasayansi wa kwanza toka kale
ambae aliweza kuchora picha Zenye mfumo wa 3D kwa kipindi hicho ambazo zilikuwa zikiimbatana na ujumbe wa siri ( secret code)
Picha
ya monalisa ni picha ya maajabu iliyojaa mauzauza ya kimtazamo kama ukitazama kwa umakini zaidi.
SIRI ILIYOFICHIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA MIATANO (500)
-
Siri kubwa iliyokuwepo katika picha hii ni kuwa ni
picha moja ambayo imeficha picha zaidi ya moja na kupitia blog hii tutazijua. Kila mwaka
picha hii hutembelewa na mamilion ya watu louvre paris.yako mambo
yanayoshangaza kwenye picha mpaka ikatoa maswali mengi, miongoni mwa mambo
niliyoyaona mimi mwandishi ni pamoja na
·
Horizon ya picha inaunganisha kutoka upande mmoja wa
picha mpaka upande mwingine
·
Hakuna mtu yoyote ulimwenguni anayefahamu hasa
zaidi huyu ni nani
·
Ukiingalia miinuko ya ardhi ndani ya picha hii ipo katika hali
ya mauzauza
·
Leonardo da vinc ananyaraka zaidi ya 7000+
lakini hakuna hata nyaraka inayomzungumzia monalisa ( ESL itajaribu kuangalia wap davinc alimzungumzia monalisa)
·
Imani iliyokuwepo kwa watu wengi kuwa huyu ni
Lisa gheradin( kitu ambacho sio sahihi)
·
Wapo wanaohisi na kuamini kuwa si mwanamke bali ni mwanaume( ESL itatoa majibu kama ni mwanamke au mwanamme) .
·
Tabasamu
linalonekana katika picha hii
limekosa majibu kwa watu wengi tu( ipo siri iliyojificha ndani ya hilo tabasamu utaijua karibuni).
TOLEO LIJALO: E.S.L ITAANZA KUCHANGANUA KILA KIPENGELE KILICHO NDANI YA HII PICHA NA MAANA ZAKE AMBAZO DA VINC ALIZIFICHA, PAMOJA NA KUJIBU MASWALI YANAOTATIZA WATU WENGI HAPO JUU. TUKUTANE TENA.