Wednesday, July 31, 2013

MADEE AKAGULIWA LISAA LIMOJA UWANJA WA NDEGE SOUTH AFRICA KWA HOFU KUWA ANA MADAWA YA KULEVYA

Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.