Mkazi wa kijiji cha Chombe katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Costantine Samson 'Siwale' (60) ameuawa kwa kuchinjwa na mtoto wa kiume wa mdogo wake kutokana na ugomvi uliosababishwa na mgogoro wa kiwanja cha kujenga nyumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema mauaji hayo yalitokea Julai 16, mwaka huu na kumtaja mtuhumiwa wa mauaji kuwa ni Lige Claudi.
Kwa mujibu wa Mwaruanda, mtuhumiwa alichukua panga na kumjeruhi baba yake mdogo kichwani na kusababisha kupoteza fahamu na damu nyingi na kisha akatumia panga hilo kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake.
Mwaruanda alisema baba mdogo na mwanawe walikuwa wakigombea kiwanja hicho ambacho kiliachwa na marehemu baba mzazi wa mtuhumiwa huku kila mmoja akidai ndiye mwenye uhalali wa kujenga nyumba hapo. Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka na anatafutwa na polisi.