Tuesday, July 23, 2013

GERARDO MARTINO KOCHA MPYA WA FC BARCELONA

FC Barcelona imefikia makubaliano rasmi kumsaini Gerardo Martino kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, kwa mujibu wa mtandao rasmi wa FC Barcelona.
Kilichobakia kwenye makubaliano hayo ni kusaini mkataba baada pande zote mbili kukubalina kila kitu. 
Ratiba rasmi ya kuwasili kwake Nou Camp, utiaji saini wa mkataba na kutambulishwa rasmi itatangazwa msaa kadha yajayo. 

Gerardo ambaye anajulikana kama ‘Tata’, alizaliwa jijini Rosario (Argentina) November 20, 1962. Ana uzoefu mkubwa wa soka la America ya Kusini, kwanza kamamchezaji na baada kama kocha, kazi yake ya mwisho ilikuwa kuiongoza klabu yaNewell's Old Boys, ambao alishinda nao ubingwa wa mwaka huu.


Gerardo Martino anakuwa kocha wa nne raia wa Argentina kuifundisha FC Barcelona baada ya Roque Olsen, Helenio Herrera na César Luis Menotti