Sunday, July 14, 2013

DK. CHENI ABARIKI MABADILIKO YA LULU

Msanii wa filamu Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amesema anamtakia mafanikio mema kinda la filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kujitangaza kuwa amebadilika
Akizungumza na paparazi wetu, Dk. Cheni alisema  amefurahi kusikia mikakati ya Lulu na kumsihi ajitahidi kuishi hivyo ili aweze kufikia malengo yake kama alivyojipangia.
“Kwanza nampongeza na namuombea kwa Mungu atimize malengo yake. Ni jambo zuri kama ameamua kujikita katika kazi zaidi ya kitu chochote,” alisema Dk. Cheni.