Friday, July 5, 2013

"BILA CHAPAA HAUJALIFAIDI PENZI LANGU, SIPENDI WANAUME SURUALI KAMWE"....JINI KABULA


Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Kabula alisema anajua kupenda ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao ni wanaume ‘suruali’.
“Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo, wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao zaidi ya kuonesha wana wivu kweli na wakipishana kidogo tu kipigo kinatembea, mimi wananikera sana,” alisema Kabula.