Tuesday, July 23, 2013

AJALI:DALADALA YANUSURIKA KUINGIA MTARONI


 Abiria wakiteremka baada ya kunusurika katika ajali.
Kondakta akibishana na dereva wa lori baada ya gari lake kunusurika kuingia mtaroni.

WASAFIRI wa basi lipigalo ruti za Ubungo - Mbagala walijikuta katika hekaheka ya kuokoa roho zao mara baada ya gari lao kunusurika kuingia mtaroni baada ya kusukumwa na lori.

Tukio hilo lilitokea barabara ya Mandela karibu na kituo cha mabasi Buguruni Sheli jijini Dar, ambapo chanzo chake kilibainika kuwa ni haraka za dereva wa basi hilo aliyetaka ‘kuli overtake’ lori moja lililokuwa katika mwendo kasi na kusababisha basi hilo kusukumwa na kidogo liingie mtaroni.

Kwa hofu, abiria wa gari hilo walinaswa wakigombea kushuka jambo ambalo walifanikiwa bila kusababisha majeraha kwa wasafiri hao.

Hata hivyo basi hilo lilifanikiwa kutoka salama huku likiwa limevunjika kioo cha upande wa kulia na kubonyea kidogo upande wa dereva.