Prof. Ibrahim Lipumba
Dar es Salaam.
Katibu wa
Jumuiya na taasisi za kiislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda anayedaiwa
kupigwa risasi na polisi mkoani morogoro mara baada ya kumalizika
mhadhara aliokuwa akihutubia, amelazwa chini ya uangalizi katika
hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Taarifa
za kulazwa kwa kiongozi huyo zimetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alikwenda kumjulia hali hii
leo.
Sheikh Ponda Issa Ponda
Prof.
Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
mara baada ya kumtembelea katika wodi ya dharura katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili amesema tukio hilo ni miongoni mwa matukio mabaya
yanayodaiwa kufanywa na vyombo vya dola ambayo hayana budi kudhibitiwa
kwani yanaweza kuwa na madhara kwa ustawi wa taifa.

"Cama cha
Cuf kinasikitishwa sana na kufadhaishwa na Mwendelezo wa vitendo vya
kikatili vya mauaji ya raia yanayo fanywa na jeshi la polisi kwa
kisingizio cha kulinda amani ya nchi, huu utaratibu au sera ya piga tu
tumechoka itatufikisha pabaya alisema Lipumba.
Aidha
Prof. Lipumba Amemwomba Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini inspekta Jenerali Saidi Mwema kuhakikisha kuwa matukio ya kupigwa
risasi wananchi wasiokuwa na silaha yanakomeshwa lakini pia wanaohusika
kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
Rais Jakaya Kikwete
Hata
hivyo Prof.Lipumba amevitahadharisha vyombo vya dola hususan jeshi la
polisi kuhakikisha kuwa linaondoa vizingiti vya kupatiwa matibabu sheikh
Ponda ,ambapo pia amewataka waislam pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa
na subira wakati sheikh ponda akiendelea kupatiwa matibabu.