WATU wanne wa familia moja wamefariki na wengine 13
wamelazwa hospitalini kutokana na kula chakula chenye sumu
wakati wa sikukuu ya Idi el Fitri.Watu hao wamelazwa
wakati wa sikukuu ya Idi el Fitri.Watu hao wamelazwa
Kituo
cha Afya cha Lusewa wilayani Namtumbo na Hospitali ya
Serikali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO).
Kamanda wa Polisi Mkoa
Deusidebit Nsimeki, alisema tukio hilo
lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 7:00. Kamanda Nsimeki,
alisema siku hiyo
kabla ya tukio, Salum Mumba, alinunua samaki
aliyepeleka nyumbani kwa ajili ya
sikukuu ya Idi.Kamanda
Nsimeki alisema katika tukio hilo Polisi wanamshikilia
mtu mmoja ambaye hakutaka
kumtaja jina ambaye atasaidia polisi
kwenye upelelezi wake.
Alisema baada ya kula
chakula hicho, haikuchukua muda mrefu
mtoto alianza kuumwa naye baadaye
alifariki dunia. Baadaye
watoto wawili walianza kuumwa na kufariki. Watu
wengine 13
walianza kuumwa baadaye majirani walipata taarifa kuwakimbiza
watu
hao hospitali.
Aliwataja waliolazwa katika
kituo cha afya cha Lusewa kuwa ni
Tazamio Mumba, Zidani Mumba, Ramadhani Mumba
na Zahara
Mumba wote wakazi wa kitongoji Tulieni B.
Waliolazwa katika hospitali
ya Mkoa wa Songea kuwa ni Gairi
Mumba, Zamoni Mumba, Fatuma Rashidi, Samidu
Mumba, Asha
Omary na Sharifa Mumba.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi ya Hospitali ya Mkoa Songea Dkt.
Benedictor Ngaiza alisema wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo hali zao zinaendelea
vizuri.